
Trump amesema virusi hivyo vimeipiga Marekani kwa nguvu zaidi ya mashambulio ya mambomu ya Japani katika Bandari ya Pearl katika Vita vya Pili vya Dunia ama shambulio la kigaidi la 9/11 miongo miwili iliyopita.
Utawala wa Marekani kwa sasa unaangazia hatua za adhabu ambazo inaweza kuichukulia Uchina kwa nmana ambavyo walilishughulikia janga hilo katika siku za awali.
Uchina hata hivyo inasema kuwa Marekani inataka kuitumia kama njia ya kuficha mapungufu yao ya nmana gani wamelishughulikua janga hilo.
Toka janga hilo lilipuke katika Mji wa Wuhan mwezi Disemba, virusi vya corona tayari vimeshathibitishwa kuwapata zaidi ya watu milioni 1.2 na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 73,000 nchini Marekani pekee.
Je Rais Trump amesema nini?
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ikulu yake Tump amesema: "Tumepatwa na shambulio kubwa zaidi kuwahi kutokea nchini kwetu.
"Shambulio hili ni baya zaidi ya la Bandari ya Pearl. Hili baya zaidi ya la Kituo cha Biashara cha Dunia (9/11). Hatujawahi kupatwa na shambuli kama hili.
"Na halikutakiwa kutokea. Lingeweza kuzuilika kwenye chanzo chake. Lingeweza kuzuiliwa na Uchina. Lingeweza kuzuiliwa kwenye chanzo chake, lakini hilo halikufanyika."
Alipoulizwa iwapo analiona janga hilo kama shambulio la kivita kutoka Uchina, Trump alijibu kuwa kwa sasa adui wa Marekani ni mlipuko wa virusi na si Uchina.
"Ninamchukulia huyu adui asiyeonekana [virusi vya corona] kama vita," amesema. "Sipendi kabisa jinsi gani alifika hapa, kwa kuwa kulikuwa na uwezekano wa kuzuia."

- Je ni kina nani wanaofadhili WHO, na zipi athari za Trump kulinyima ufadhili shirika hilo?
- Trump apendekeza watu kuchomwa sindano za kemikali
- Je, ni dawa gani hii inayopigiwa upatu na Trump 'kutibu' coronavirus?

Nani mwengine kwenye safu ya Trump anayekosoa Uchina?
Mzozo mkubwa baina ya Washington na Beijing umezidi kukolezwa jana Jumatano baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo aliporejelea mashambulizi yake dhidi ya Uchina kwa kuwatuhumu kuficha taarifa za janga hilo.
Bado ameendelea kusema kuwa "kuna Ushahidi mwingi" unaoonesha kuwa virusi hivyo vilitengenezwa kwenye maabara moja nchini Uchina japo madai hayo hayajathibitishwa.
Hata hivyo, amekiri kuwa bado kuna mashaya wapi virusi hivyo vilipochipukia
"TKauli zote mbili hizo ni sahihi" Pompeo ameiambia BBC, "Hatuna uhakika wa moja kwa moja virusi vimechipukia wapi lakini kuna Ushahidi wa kutosha kuwa vilitengenezwa maabara moja nchini China."
Shirika la Habari la Serikali ya China limemtuhumu Pompeo kwa kusema uongo.
Hata hivyo moja ya madaktari wanaoheshimika katika Serikali ya Trump Dkt Anthony Fauci amesema kuwa Ushahidi bora zaidi unaonesha kuwa virusi hivyo havikutengenezwa maabara.
Pia unaweza kusoma:
0 Comments